SectionsOffertoryEe Bwana Uisikie Haki

Ee Bwana Uisikie Haki

Ordinary TimeOffertory
Chorus

Ee Bwana uisikie haki, usikie haki

Utege sikio lako Bwana, kwa maombi yangu (Bwana)n{ Usikilize maombi yangu yasiyotoka katika,

Yasiyotoka katika midomo ya hila } *2

Verse 2

Nyayo zangu zimeshikamana, zimeshikamana na njia zako,

Hatua zangu haziku, hazikuondoshwa.

Verse 3

Ee Mungu nimekuita wewe, kwa maana wewe utaitika,

Utege sikio lako nisikie mimi.

Verse 4

Unifiche chini ya uvuli, chini ya uvuli wa mbawa zako

Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.