SectionsEucharistEe Bwana Sistahili

Ee Bwana Sistahili

Ordinary TimeEucharist
Chorus

{ Ee Bwana, sistahili

Sistahili ee Bwana uje moyoni mwangu } * 2n{ Lakini sema neno Bwana sema nenon(neno tu)

Nami nitajongea mbele kwa karamu } *2

Verse 2

Karamu ya Bwana yatupa uzima

Ni mwili wa Bwana na damu yake

Verse 3

Hiki ni chakula kutoka Mbinguni

Bwana atuita kutushibisha

Verse 4

Huu mwili wangu hii damu yangu

Njooni kwangu nami nitawalisha

Verse 5

Siku zote Bwana atulisha sisi

Kwa chakula bora kutoka Mbinguni

Verse 6

Atukuzwe Baba atukuzwe Mwana

Atukuzwe Roho Mtakatifu daima yote