SectionsBible ProcessionEe Bwana Ninakuja

Ee Bwana Ninakuja

Ordinary TimeBible Procession
Chorus

Ee Bwana ninakuja mbele ya altare yako

Unipokee Bwana wangu nikutumikie

Ninajitolea kwako maisha yangu yote

Nakuomba unitakase niwe mtumishi wako

Hayana haja ya dunia nikutumikie wewe

Unijaze roho wako niwe mtumishi mwaminifu

Verse 2

Ninakuja kwako Bwana, unipokee Muumba wangu

Nahitaji wito ewe Bwana Mungu wangu

Unijaze roho wako nikutumikie

Verse 3

Bila msaada wako, peke yangu hakika siwezi

Nahitaji nguvu yako Bwana inisaidie

Unijaze roho wako nikutumikie

Verse 4

Ni vikwazo vingi sana, vya shetani vinavyonisonga

Nahitaji neema yako ili nivishinde vyote

Unijaze roho wako nikutumikie