SectionsExitDunia Mti Mkavu

Dunia Mti Mkavu

Marian,Ordinary TimeExit
Verse 1

Dunia ni mti mkavu, nimeona nimeamini

Wanaosema ni wajanja sasa nao wapagawa

Chorus

Ukiuliza mashariki - sijui

Ukiuliza magharibi - sijui

Kaskazini na kusini - sijui

Hata nao pia wanasemezana - sijui

Dunia imebadilika - sijui

Na sisi tutakwenda wapi - sijuin

Hiki kiza chatikisa dunia yetu

Twaomba Baba tuonee huruma utuokoe *2

Verse 3

Mambo mengi yabadilika huku kule kwashangaza

Jibu limekuwa 'sijui' amani yatatanisha

Verse 4

Tumuombe Mwenyezi Mungu ashushe baraka zake

Ili tuishi kwa amani, dini zote zipendane

Verse 5

Twaiombea nchi yetu, Baba Mungu uilinde

Uiepushe na majanga na maradhi ya kutisha