Chorus
Usipange foleni kwenye duka la shetani
Utauziwa dhambi faida yake mauti
Nenda ukajipange dukani kwa Bwana Yesu
Utapata kibali cha kuingia mbinguni
Verse 2
Enyi wavuta bangi, na madawa ya kulevya
Mbona mmejipanga katika duka la shetani
Verse 3
Na ninyi wala rushwa, makahaba na wachawi
Mbona mmejipanga katika duka la shetani
Verse 4
Duka lake shetani limejaa vitu vingi
Tena vyapendeza sana na kuuvutia moyo
Verse 5
Ramani ya mbinguni nenda kwake Yesu
Ramani ya kuzimu shetani ndiye mchoraji
Verse 6
Mnaofunga ndoa katika jinsia moja
Nanyi mmejipanga katika duka la shetani
Verse 7
Mavazi ya aibu dada zetu mwajivika
Mnaita vimini shetani anachekelea