Chorus
Chochote chochote chote
Chochote umtendeacho mwenzio,
Ujue kwamba umenitendea mimi
Verse 2
Nilipokuwa na njaa,
We ukanipa chakula
Nilipokuwa ni mgeni
We ukanikaribisha
Verse 3
Nilipokuwa na kiu
We ukanipa maji
Nilipokuwa bado ni uchi
We ukaja kunivika
Verse 4
Nilipokuwa mgonjwa
We ukaja kuniona
Nilipokuwa gerezani
We ukanitembelea