Chorus
Si sawa kuchukua chakula cha watoto (si sawa)
Na kuwatupia mbwa chakula cha watoto (lakini)
Hata mbwa hula makombo yaangukayon(kutoka) mezani mwa Bwana wao
Nami natamani kuonja chakula hikin(ulicho) waandalia wanao
Japo sifai mimi nakusihi Bwana, uniruhusu tu *2
Verse 2
Nakutamani sana, Bwana wangu (mwema),
Kujongea karamuni,
Ijapokuwa mimi sina moyo safi,
Nina njaa nina kiu niruhusu tu
Verse 3
Nimejawa na dhambi, na uchafu (mwingi),
Na nimeoza moyoni
Mawazo mabaya na matendo maovu,
Hata naona aibu, niruhusu tu
Verse 4
Nisipokupokea, mwili wako (Bwana),
Sina uzima milele
Sasa niende wapi zaidi ya kwako,
Nisamehe nipokee niruhusu tu
Verse 5
Maana ulikuja, duniani (kwao),
Wenye dhambi kama mimi
Ulikula nao hata ukafa nao,
Na mimi nakuhitaji niruhusu tu