SectionsEucharistChakula Bora

Chakula Bora

Eucharist
Verse 1

Sasa ninahisi harufu ya chakula,

Harufu nzuri tena ya kipekee,

Kweli ninahisi harufu ya kinywaji

Harufu nzuri tena ya kipekeen

Chorus

Amkeni wapenzi (twende) kule sebuleni

Tuandamane sote (twende) tufike mezani

Tukamwone mpishi (huyo) aliye imara,

Tukamwone ni nani huyo anayesisimua lo, n(kumbe ni Yesu ametuandalia mazuri

Tujitakase tushiriki chakula bora *2)n

Verse 3

Kati ya wapishi wote ulimwenguni

Sijawahi ona mpishi kama Yesu,

Anayeandaa chakula cha thamani

Kinachodumisha uhai siu zoten

Verse 4

Kati ya wafalme wote ulimwenguni

Sijawahi ona aliyefanikiwa

Kuwaandalia watu wote karamu

Akawashibisha pasipo ubaguzin