Bwana Ninakuita
Ordinary TimeBible Procession
Verse 1
Bwana ninakuita kwa maana utaitika
Utege sikio lako Mungu wangu
Bwana usikilize sala nayo maombi yangu
Unifanye niwe chombo cha amani
Chorus
Unifanye niwe chombo cha amani ee Bwana
Unifanye mimi niwe nuru ya mataifa
Mashariki magharibi, niende
Niihubiri imani ya Bwana
Kaskazini na kusini niende
Niuhubiri upendo wa Bwanan{ Nitembee pande zote mimi Bwana, ee Bwana
Nikalitangaze neno lako kwa mataifa } *2
Verse 3
Bwana uniongoze jina lako ni fimbo yangu
Wewe ndiwe ngao yangu niendapo
Bwana upendo wako nashindwa kusimulia
Na ninakupenda sana Mungu wangu
Verse 4
Bwana uniongoze niyashinde majaribu
Wewe ndiwe ngao yangu niendapo
Bwana watesi wangu tazama ni wengi sana
Niongoze nimshinde mwovu shetanin