SectionsExitBwana Ni Mchungaji

Bwana Ni Mchungaji

Ordinary TimeExit
Verse 1

Bwana ni mchunga, sitahitaji.

Majani mabichi, malisho yangu.

Ananinywesha maji matulivu

Atanirudisha nikipotea

Verse 2

Nipitapo bondeni mwa mauti,

U mlinzi wangu, sitaogopa.

Fimbo lako latosha kunilinda.

Ukinifariji sina hasara.

Verse 3

Kati ya mateso meza waandaa

Na kikombe changu kinafurika

Umenipaka kichwani mafuta.

Nitaulizaje zaidi kwako.

Verse 4

Wema na fadhili vinifuate

Siku zangu zote, hata milele.

Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana.

Katika ufalme wa pendo lake.n