SectionsExitBwana Nakupenda

Bwana Nakupenda

Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary TimeExit
Chorus

Bwana nakupenda we Mungu wangu

Pembe ya wokovu na nguvu yangu

Wewe ndiwe mwamba na jabali langu

Nakimbilia kwako Mwokozi wangu

Bwana ndiye kinga na ngao yangu

Yeye ndiye mwamba na ngome yangu

Bwana ndiye kinga na ngao yangu

Sitaogopa nimwogope nanin{Kwa hiyo nitamwita astahili sifananiokoe na adui zangu *2

Verse 2

[t/b] Asifiwe Mungu aliye hai atukuzwe Mungu wokovu wangun[s/a] Asifiwe mwamba wa usalama, atukuzwe kati ya mataifan[t/b] Ampa mfalme wokovu wote, wokovu mkuu ampatian[s/a] Amfanyia fadhili masihi humjalia mteule waken[t/a] Kwa hiyo nitaliimbia sifa jina lako Mungu wangu

Verse 3

Kamba za kifo zilinizingira, maangamizi yalinivamia

Kamba za kuzimu zilinisonga, mitego ya kifo ilinikabili

Katika tabu nilimwita Mungu nilimlilia anisaidie

Aliisikia sauti yangu hekaluni mwake alisikia

Kilio changu kilimfikia masikioni mwake

Verse 4

Hapo ndipo dunia ikatetemeka ilihangaika na kutikisika

Misingi ya milima ikayumbayumba Mungu alikuwa amekasirika

Moshi ulishuka puani mwake moto uvunjao kinywani mwake

Aliinamisha anga akashuka chini na wingu jeusi miguuni pake

Makaa mengi ya moto yakalipuka kutoka kwake

Verse 5

Mungu alinguruma kutoka mbinguni mkuu akatoa sauti yake

Alipulika giza mawingu mazito yaliyojaa maji yalimzunguka

Huko mawinguni makaa ya moto mvua ya mawe zikatokea

Alirusha umeme ukawapiga maadui zake wakatawanyika

Hapo ndipo bahari na dunia zilipoonekana

Verse 6

Mungu alinyoosha mkono wake kutoka juu akanichukua

Katika maji mengi alininyanyua akanitoa kwa adui zangu

Tegemeo langu ni Bwana Mungu aliniokoa na adui zangu

Walioniwinda aliwatisha aliwakemea wakapotea

Amenitoa hapo akanipeleka palipo na nafasi