SectionsExitBwana Ametukuka Sana

Bwana Ametukuka Sana

Ordinary Time,MarianExit
Verse 1

Ndipo Musa na (wana) wa Israelinwakamwimbia Bwana wakinena

Chorus

Nitamwimbia Bwana kwa kinywa changu

Kwa maana ametukuka sana

Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini

Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu

Naye amekuwa wokovu wangu

Yeye ni Mungu wangu na baba yangu nami nitamsifu

Verse 3

Bwana ni mtu wa vita, mtu wa vita

Bwana ndilo jina lake jina lake

Magari na jeshi lake Farao amewatupa baharini

Maakida yake wateule wamezama bahari ya shamu

Vilindi vimewafunikiza walizama vilindini kama jiwe

Verse 4

Bwana mkono wako wa kuume

Umepata fahari ya uwezo

Bwana mkono wako wa kuume wawatesatesa adui

Kwa wingi wa ukuu wawangusha chini wanaokuondokea

Verse 5

Utawaingiza Bwana na kuwapanda

Katika mlima wa urithi wako

Mahali pale ulipojifanyia Bwana ili upakae

Pale patakatifu ulipopaweka imara Bwana

Bwana kwa mikono yako

Bwana atatawala milele yoten

Ndipo Musa…..