Chorus
Bwana amejaa huruma na neema
Haoni hasira upesi ni mwingi wa fadhili
Maana Mbingu zilivyoinuka juu ya nchi
Kadiri ile ile, rehema zake ni kuu kwa wamchao
Verse 2
Ee nafsi yangu umhimidi Bwana
Na vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi Jina lake Takatifu
Ee nafsi yangu umhimidi Bwana
Wala usizisahau fadhili zake zote
Verse 3
Akusamehe maovu yako yote
Akuponya magonjwa yako yote
Aukomboa uhai wako na kaburi
Akutia taji la fadhili na rehema
Aushibisha neema uzee wakon
Verse 4
Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki
Na hukumu kwa wote wanaoonewa
Alimjulisha Musa njia zakenna wana wa Israeli matendo yake
Wana wa Israeli matendo yake