SectionsExitBwana Aliridhika Kumchubua

Bwana Aliridhika Kumchubua

LentExit
Chorus

Bwana aliridhika kumchubua, amemhuzunisha

Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu, dhabihu kwa dhambinn{Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi

Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake } *2

Verse 2

Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake

Na kuridhika, na kuridhika

Naye atayachukua maovu yao

Verse 3

Kwa maarifa yake mtumishi wangu

Ataridhika, ataridhika

Naye atafanya wengi kuwa wenye haki