SectionsEucharistBlessed Assurance (Kiswahili)

Blessed Assurance (Kiswahili)

Eucharist
Verse 1

Ndiyo dhamana, Yesu wangu

Hunipa furaha ya mbingu

Mrithi wa wokovu wake

Nimezawa kwa roho yake

Chorus

Habari njema, raha yangu

Yesu ndiye mwokozi wangu *2

Verse 3

Kumsalimu moyo wangu

Mara namwona raha yangu;

Aniletea malaika

Wananilinda, taokoka

Verse 4

Sina kinyume, nashukuru

Mchana kutwa huja kwangu;

Usiku kucha kuna nuru;

Mwokozi mbwangu, ndimi huru

Verse 5

Hali na mali, anitwaa!

Mara namwona anifaa

Nami nangoja kwa subira;

Akiniita nije mara