Bendera ya Kristu yapepea, na tena yaongoza jahazi
Ukiwa ndani ya Kristu ucheze
Marimba cheza hima kikristu (Bendera)
Ni bendera ya Kristu na hata Bwana,
Yatuonyesha njia ya ukweli Bwana
Yapepea inatuongoza kwa Baba mbinguni juu
Bendera bendera yenye msalaba wa ushindi
Ushindi ushindi kwa kuteswa kwake tumepona
Bendera, bendera inatuongoza kwake Baba
Yanipa, yanipa kila tumaini na ushindi
Bendera bendera katikati yake ni msalaba
Msalaba msalaba alama ya Kristu mshindaji
Msalaba msalaba mti wa thamani wa bendera
Ni mti ni mti bendera kwa huo yapepea
Bendera bendera msalaba wake ni mwekundu,
Ni damu ni damu ya Mwanakondoo mshindaji
Kondoo kondoo aliyetolewa ni sadaka
Sadaka sadaka kwa kuchinjwa kwake tumepona
Bendera bendera pembe ni jeupe inang`ara
Ishara ishara ya utakatifu mlovaa
Bendera bendera haiteteleki yaongoza
Ni njia ni njia yenye uhakika wa mbinguni