Beba Mikononi

Ordinary TimePresentation of Gifts
Verse 1

Tusimame ndugu twende kwake Bwana (kweli)

Usisite ndugu amka twende hima

Chorus

Beba mikononi (mwako) uliyojaliwa

Peleka kwa Bwana, upate Baraka

Verse 3

Peleka kwa moyo, moyo wa mapendo (kweli)

Peleka kwa Bwana uliyojaliwa

Verse 4

Sadaka ya fedha, fedha za mifuko (ndugu)

Amka upeleke mezani kwa Bwana

Verse 5

Mavuno mifugo, ni mali ya Bwana (kweli)

Tupeleke kwake atazipokea

Verse 6

Mkate divai tupeleke kwake (leo)

Tupate baraka mbele zake Bwana

Verse 7

Twende ndugu twende, mbele zake Bwana (twende)

Tupeleke nafsi zetu kwake Bwana