Chorus
{ Basi mkiwa mmefufuliwa, pamoja na Yesu Kristu
Yatafuteni yaliyo juu Kristu aliko
Ameketi mkono wa kuume,nmkono wa kuume wa Mungu } * 2
Verse 2
Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi
Kwa maana mlikufa na uhai wenu
Umefichwa pamoja na Kristu katika Mungu
Verse 3
Kristu atakapofunuliwa, aliye uhai wetu
Ndipo na ninyi mtafunuliwa
Pamoja naye pamoja naye katika utukufun
Verse 4
Lakini sasa Kristu amefufuka, amefufuka katika wafu
Limbuko lao waliolala, maana mauti ililetwa na mtu
Kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu