SectionsExitBaragumu La Maria

Baragumu La Maria

Ordinary TimeExit
Verse 1

Nawakaribisha viumbe wa dunia tumuimbie -

Nawakaribisha viumbe wa dunia tumuimbie

Kwa kuwa wokovu wetu umepitia, tumboni mwake

Ndiye simu ya neema toka kwa Baba, kuletwa kwetun

Chorus

Tumpigie ngoma, vinanda na baragumun{Mama Maria (salamu)

Mama wa Yesu (Maria)} *4

Pigeni kelele za shangwe, shangilia

Verse 3

Mnaokubali kwamba Yesu ni Bwana na Mungu wenu

Hebu fikirini ana thamani gani, mzazi wake

Mama pekee aliyejaliwa mimba, kutoka juu

Chorus

Tumpigie ngoma vinanda na baragumun{Mama Maria (salamu)

Mama wa Yesu (Maria)} *4

Kwa ngoma na matarumbeta furahia

Verse 5

Alimbadilisha nepi Bwana wetu Mwokozi wetu

Akamuogesha tunayemuabudu, mwana wa Mungu

Anajua kula yake na vaa yake, na lala yake

Chorus

Tumpigie ngoma vinanda na baragumun{Mama Maria (salamu)

Mama wa Yesu (Maria)} *4

Kwa kinanda cha nyuzi kumi, sherekea

Verse 7

Ulimwengu ungeijua siri hii, na tungepona

Sote tungekubali kusali rozari, tungeokoka

Amani ingepatikana duniani, tungefurahi

Chorus

Tumpigie ngoma vinanda na baragumun{Mama Maria (salamu)

Mama wa Yesu (Maria)} *4

Kwa filimbi na kwa nzumari, changamka