SectionsExitBaba Mama Na Watoto

Baba Mama Na Watoto

Ordinary Time,BaptismExit
Verse 1

Baba mama na watoto wao ni familia kamili

Na hawa wote ni muhimu, kujenga kanisa la Yesu

Katika kujenga Kanisa la Yesu ujenzi huanza nyumbani

Na kupeana majukumu, kila mmoja na lake

Chorus

Mama awe katekista, na baba awe padre

Mama awe katekista, na baba awe padren{Watoto wawe ubao[ubao] kufundishia wengine

Ili wengineo wajifunze, kuishi maisha mema} *2

Verse 3

Mama awe katekista maana yeye ndiye mwalimu

Kwa kuwa ana huruma na ni mlezi wa watoto

Awafundishe mema yote, upendo sala na bidii

Na kuwafundisha nidhamu kwa wenyewe na kwa wengine

Verse 4

Baba yeye awe padre, tena yeye ndiye mchungaji

Ashirikiane naye mama, watoto wao kuwalea

Awe mwelekezaji pale watoto wanapopotoka

Ili waweze kujenga familia iliyo bora

Verse 5

Watoto wawe ubao ubao, kufundishia wengine

Kwa tabia zao nzuri na uadilifu mwema

Watakuwa ni mfano bora na kielelezo sawia

Hiyo ndiyo familia ya kumpendeza Mungu

Verse 6

Baba mama na watoto wao ni familia kamili

Na hawa wote ni muhimu, kujenga kanisa la Yesu

Katika kujenga Kanisa la Yesu ujenzi huanza nyumbani

Na kupeana majukumu, kila mmoja na lake