SectionsEntranceAsiregeee Moyowe

Asiregeee Moyowe

LentEntrance
Verse 1

Asiregee moyowe, asitoke machozi

Akikumbuka Mungu wake, kwa yakenmakombozi, mtoa roho msalabani,nmtaka kufa mwenyewe, kwa sababunkumpendani, nani mfunga moyowe.

Verse 2

Bustani mle Getsemani, amwona Mungu

Baba, je mtu Mungu ana nini, nguvu zakenni haba, Bwana wangu waziona, dhambinza binadamu mwili wako umetona,nkama jasho la damu.

Verse 3

Salamu Rabi salamu, anena Yudanmbaya, mwenye moyo wake mgumu,nambusu pasi haya aliwaambia basi,nntakayembusu ndiye, mtwaeni na kwa upesi,

Yuda nani ni siye.

Verse 4

Yuda nani sio yeye, aliyetenda dhambi,

Tukimkosa Mungu Baba, kumdharaunnaye mwana, tukimsikitisha Roho, tunvipofu kama Yuda, tunatupa neema yake,nitokayo kwake Yesu.

Verse 5

Wote ni kupiga mbio, mitumewe pamoja,

Wamtia mikono yao, askari walokuja

Wampeleka hukumuni, aamuriwe na mtu

Atokaye uwinguni, mwanzi mkuu wa watu.

Verse 6

Mtume Petri amkanusha, amenena simjui

Uhodari umekwisha, machoye hainui

Pilato amwona Bwana, hakukosa ta neno

Asema sioni dhambi, lakini ni mwoga mno.

Verse 7

Hathubutu kumwachia, sioni nanawanmikono, mkimtaka Yesu muueni,nla mwanzi hilo neno mara askarinwamwanza, ni kupiga kelele, kumchekanna kumchokoza, mwenye mema milele