Asante Mungu Mwenyezi
Ordinary Time,BaptismThanksgiving
Verse 1
Asante Mungu Mwenyezi, asante (asante)
Muumba mbingu na nchi, asanten{ Nakushukuru Mungu wangu kwa mema yako yote (leo)
Milele hata milele nitaimba sifa zako (mimi)
Nitaimba sifa zako kwa shangwe } * 2
Verse 2
Kwa wingi wa fadhili zako nakushukuru Bwana
Kwa wingi wa rehema zako asante Mungu wangun
Verse 3
Umeniumba mimi Bwana ukanipa akili
Ninakushukuru ee Mungu kwa moyo wangu wote
Verse 4
Nitaziimba sifa zako katika kusanyiko
Nitatanganza Neno lako milele na milele