SectionsThanksgivingAsante Kwa Wema

Asante Kwa Wema

Ordinary Time,MarianThanksgiving
Verse 1

Bwana alinitendea mambo makuu

Nilipoita jina lake aliniitikia

Alinitegemeza katika taabu zangu

Chorus

{ Asante- kwa wema wako

Asante-kwa ukarimu

Asante kwa pendo lako nashukuru } * 2

Verse 3

Bwana ameniponya na magonjwa mengi

Pia amenikinga na ajali mbaya sana

Amenitoa katika mitego ya shetani

Verse 4

Nimetafakari upendo wake Bwana

Kujivika ubinadamu na kufa msalabani

Ili nikombolewe utumwani wa shetani

Verse 5

Ni mara nyingi sana nimetenda dhambi

Lakini Bwana Yesu hakunihukumu kwa dhambi

Hakuna kama Bwana yeye ni Mungu pekee

Verse 6

Wema wake Mungu wangu hauna mwisho

Ameniandalia makao baada ya kifo

Masharti yake niwe nimetii amri za Mungu

Verse 7

Enyi ndugu zangu mlio katika Kristu

Unganeni pamoja nami kumshukuru Mungu

Ni mema mengi sana yeye ametujalia