SectionsThanksgivingAsante Bwana Kwa Ukarimu

Asante Bwana Kwa Ukarimu

Ordinary Time,MarianThanksgiving
Verse 1

Asante Bwana kwa ukarimu wako wa ajabu,

Na fadhili zako hazina mipaka,

Sina budi kusema Bwana asante

Chorus

Umenijua Bwana kabla sijazaliwa

Maisha yangu umeweka kwenye msitari

Kwa maana umenipenda, umenijali

Nakushukuru ee Bwana asante *2

Verse 3

Ninapotafakari upendo wako kwangu mimi

Na riziki zangu wanipa kila siku

Nashindwa nikulipe nini ee Bwana

Verse 4

Na mwili wangu umenipa akili ya kutosha

Kuliko wanyama utashi umenipa

Ufananishwe na nani ee Bwana

Verse 5

Uhai wangu umenipa na sasa niko hai

Wengi wamezikwa mimi bado nahema

Nikulipe nini kwa upendo wakon

Verse 6

Na marafiki ndugu jamaa Bwana umenipa

Dhiki zikinizidi wanifariji

Upendo wako Bwana unanishangaza.

Verse 7

Kwa hayo yote siwezi lipa langu shukraninna mengi bado hata siwezi kusema

Bwana unayotenda kwangu makuu