Chorus
Kwa maana angalieni sasa yametimia (yale yote)
Manabii walotabiri sasa yametokea (ona)
Verse 2
Baba atamkana mama, mama atamkana Baba
Watoto ni hivyo hivyo, tubuni tubuni sasa
Verse 3
Magonjwa yasiyopona, uasherati wazidi
Uzinzi na ubakaji, tubuni tubuni sasa
Verse 4
Vita pande za dunia, bila sababu yoyote
Watu waabudu fedha, tubuni tubuni sasa
Verse 5
Njaa nayo itazidi ukame chakula hakuna
Watu wateseka sana, tubuni tubuni sasa
Verse 6
Neno litahubiriwa, pande zote za dunia
Watu wamfuate nani, tubuni tubuni sasa
Verse 7
Manabii wa uongo, watazunguka dunia
Watawapotosha watu, tubuni tubuni sasa
Verse 8
Tubuni tubuni sasa, tubuni tubuni sasa