Angalia Jinsi Mkulima
LentPresentation of Gifts
Chorus
{Angalia jinsi mkulima anavyofurahi-ya, kuyachuna matunda (yale) yalivyo vizuri katika bustani yake}*2
Na pia kuyatupa yale mabovu mbali
Na kuyaacha yaliyo mabichi ili yapate kuiva vizurinili aweze kuyachambua tena
Verse 2
Vivyo hivyo Mungu hufurahia kuwaita kwake wale walioa safi
Na kuwapa nafasi ya kutubu wale wenye dhambi
Verse 3
Ni wajibu kwangu mimi na wewe, kutubu kwani hakuna ajuaye siku
Wala saa ambayo Mungu Baba atamwita kwake
Verse 4
Ewe ndugu yangu unafikiria nini kuingia katika jubilei
Ya miaka elfu mbili ukiwa na mzigo wa dhambi
Verse 5
Yafaa nini mtu kupata raha zote za dunia ambazo ni za muda
Na kutupwa katika moto ule wa milele yote
Verse 6
Mimi na wewe tutumie nafasi hii tuliyopewa tutubu dhambi zetu
Mtu asijeijutia siku atakayoitwa