Anameremeta
Anameremeta sana, anameremeta kama lulu
Hakika ni nyota ya asubuhi
Huyu ndiye yule mama, mama yake Bwana Yesu Kristu
Hakika ni mama Mama wa Mungu
Kwa nini tusimshagilie, (tena) tukirukaruka kwa furaha(pia)
Na vigelegele tuvipige tukimshangilie mama Maria
Kwani kupitia kwake mama (huyo) ukombozi wetu umefika (kwetu)
Kwa nini tusimwite Yesu tukiegemea kwake Maria
Mama huyu mama gani, mama mwenye moyo safi
Mama aliyeleta nuru ya kuangaza kote
Mama anameremeta, tena anang'ara sana
Anang'ara kama lulu, lulu ya thamani kubwa
Watakatifu Mbinguni wanasifu Maria
Nao wanameremeta wakiitazama nuru
Mama huyu ni wa nuru, ni nuru ya ulimwengu
Tena anang'ara sana pia anaangaza
Maria naye Yosefu, walokuwa naye Yesu
Nao wanang'ara sana pia wanameremeta
Nasi tunaomsifu kuwa Maria ni Mama
Nasi tunang'ara sana pia tunameremeta