Chorus
Amri mpya nawapa, nawapa mpendane
Amri mpya nawapa, nawapa mpendanen{ Kama vile nilivyowapenda nyinyi
Mpendane vivyo hivyo} *2
Verse 2
Wala hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu
Wa mtu kutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake
Verse 3
Kama vile Baba alivyonipenda na nilivyowapenda nyinyi
Kaeni katika pendo, kaeni katika pendo langu
Verse 4
Nimewaambia haya ili furaha yangu iwe ndani yenu
Nayo furaha yenu furaha yenu itimizwe