SectionsEntranceAmkeni Tufanye Shangwe

Amkeni Tufanye Shangwe

Ordinary Time,MarianEntrance
Chorus

Amkeni wapenzi tufanye shangwen(Kweli) Hekaluni mwa Mungu wetu

Amkeni wapenzi tufanye shangwe n(Kweli) Hekaluni mwa Mungu wetun{Kwa vigelegele, na kwa makofi,

Kwa machezo pia kwa nderemo

Tumsifu Yaweh Jehova leo asubuhi} *2

Verse 2

Waumini wote wenye moyo safi njooni tuingie kwa Bwana

Njooni tuabudu njooni tusujudu pia tupigeni makofi

Njooni tuimbeimbe tuchezecheze turukaruke leo

Njooni hekaluni mwa Bwana tufurahi na tushangilie

Verse 3

Enyi Baba njooni tusali pamoja ndani ya nyumba yake Baba

Enyi mama njoni pigeni kelele mbele za Bwana Mungu wetu

Njooni tuimbeimbe tuchezecheze turukaruke leo

Njooni hekaluni mwa Bwana tufurahi na tushangilie

Verse 4

Ameumba mbingu ameumba nchi ameumba viumbe vyote,

Bahari ni yake mito na milima ahimidiwe Mungu wetu

Njooni tuimbeimbe tuchezecheze turukaruke leo

Njooni hekaluni mwa Bwana tufurahi na tushangilie