Chorus
Amka ewe usinziaye, amka ewe usinziaye
Amka, amka, fungua macho, amka
Pesa ni kitu cha kushangaza
Imezitega nyoyo za watu tazama,
Tazama uaminifu hakuna
Imejenga matabaka kwa maskini na matajiri, pesa
Imekuwa ni kitanzi, inafilisha hata sheria, pesa
Inagombanisha ndugu kwa ndugu pesa (tena)
Imekuwa ndio mzizi wa tamaaa
Lakini ajabu ni kwamba,
Pesa kamwe pesa kamwe,
Haitanunua mbingu ee Mungu
Kama matajiri watamiliki hewa,
Maskini wangekuwa wapi
Kama matajiri wangemiliki mbingu,
Maskini wangekosa hakin
Verse 2
Pesa ni rafiki kwenye shida zako
Lakini pesa ni adui kwenye raha zako
Verse 3
Pesa yabadili msimamo wako
Tazama pesa ni mbolea hustawisha dhambi
Verse 4
Pesa ni mtego kwa imani yako
Pesa ni mtego kwa imani yako
Na tena pesa ni kioo kwa tabia yako