Amin kweli, nawaambieni mwanitafuta
Si kwa sababu mlikuka ule mkate
Si kwa sababu mliziona zile ishara
Bali kwa sababu mlikula mkashiba
Amin, amin nawaambieni
Kuna chakula kinachowafaa
Nacho chakula ndicho kile cha
Uzima wa milele
Msikitendee kazi chakula kinachopita
Bali chakula kidumucho milele
Chakula musa alichowapa hakiwafai
Kweli Babangu anawapa kifaacho
Kile chakula chenye uzima kweli ni mimi
Ajaye kwangu hataona njaa kamwe
Anayekula huu mwili wangu na kuinywa damu
Hukaa kwangu name hukaa ndani yake
Hicho chakula chenye uzima kweli ni mimi
Kilichoshuka toa mbinguni kwa baba
Mtu akila chakula hiki hatafariki
Bali anao uzima wa milele
Kile chakula ninachotoa ni mwili wangu
Kwa ajili ya uzima wa ulimwengu
Msipokula huu mwili wake mwana Adamu
Hamna ‘zima ndani yenu
Anayekula huu mwili wangu na kuinywa damu
Ana uzima name nitamfufua
Na mwili wangu ndicho chakula kile chakweli
Na damu yangu ndicho kinywaji cha kweli
Anayekula huu mwili wangu na kuinywa damu
Ana uzima name nitamfufua
Na mwili wangu ndicho chakula kile chakweli
Na damu yangu ndicho kinywaji cha kweli