SectionsThanksgivingAmezaliwa Masiya Wetu

Amezaliwa Masiya Wetu

ChristmasThanksgiving
Chorus

Amezaliwa Masiha wetu, hoyee hoye hoye hoye

Mwana wa Mungu mkombozi wetu, hoyee hoye hoye

Leo kazaliwa naye Maria na amelazwa

Kwenye hori la wanyama, twende tukamwone

Amekuja kwetu mwana wa Mungu kuzichukua dhambi zetu wanadamu, mkombozi wetun{ Tumsujudie Bwana Mungu,kwa vigelegele

Tucheze ngoma na kayamba tupige makofi }*2

Verse 2

Amelala manyasini, twendeni tukamwone,

Tukamsalimie Mkombozi wetu

Kwa zawadi zetu za dhahabu uvumba na manemane

Verse 3

Wachungaji waondoka, waenda Bathlehemu,

Wakamsujudie Bwana Mkombozi,

Wafurahi naye pamoja na Maria naye Yusufu

Verse 4

Malaika wamefika wengi na wa mbinguni

Tukajiunge nao tuimbe pamoja utukufu uwe

Kwa Mungu juu amani kwa watu wenye mapenzi mema

Verse 5

Tumpokee mkombozi Masiha amekuja

Ewe mtoto Yesu ishi ndani yetu, tuangaze sisi,

Kwa mwanga wako mwanga wa Mbinguni