SectionsExitAmetamalaki

Ametamalaki

Ordinary TimeExit
Verse 1

Njooni na vinanda, ngoma zeze vinubi

Tumpigie Mungu wetu muziki mtakatifu

Chorus

Ametamalaki - ametamaliki Bwana ametamalaki

Mbinguni ni yeye -

Duniani ni yeye -

Ametamaliki -

Verse 3

Malaika Mbinguni wanamsifu Mungu

Na duniani pia asifiwaye ni Mungu wa milele

Verse 4

Asubuhi mapema ndege walialia

Wakisifu pia wakishukuru kwa sauti za shangwen

Verse 5

Tazama sura yako na ya jirani yako

Muonekano huo ni mfano wake Mwenyezi Mungun

Verse 6

Uhai wetu uko mikononi mwa Bwana

Autoaye ndiye auchukuaye milele milele

Verse 7

Uwepo wake unaonekana wazi

Kwa matendo ya huruma ayatendayo kila siku