SectionsSign of PeaceAmecca Mass (Nasadiki)

Amecca Mass (Nasadiki)

Ordinary Time,MarianSign of Peace
Verse 1

Nasadiki kwa Mungu mmoja – mimi nasadiki

Ndiye Baba yetu mwenyezi -

Mwumba mbingu pia dunia -n

Chorus

Nasadiki kwa Yesu Kristu

Nasadiki ninasadiki – mimi ninasadiki

Nasadiki ninasadiki – mimi ninasadiki

Verse 3

Mwana wa pekee wa Mungu –

Aliyezaliwa kwa Baba –

Akapata mwili kwa Roho –

Kazaliwa naye Bikira –

Kasha yeye kasulibiwa –

Kwa mamlaka yake Pilato –

Kwa ajili yetu kateswa –

Akafa na akazikwa –

Verse 4

Kafufuka katika wafu –

Akapaa juu mbinguni –

Ameketi kuume kwake –

Mungu Baba yetu mwenyezi –

Verse 5

Ndipo atakapotokea –

Ili awahukumu wote –

Kwake Roho Mtakatifu –

Kwa Kanisa la Katoliki –

Verse 6

Ushirika wa watakatifu –

Ondoleo la dhambi zetu –

Nangojea ‘fufuko wa miili –

Na uzima wa milele –