Alidharauliwa Na Kukataliwa
Alidharauliwa na kukataliwa kukataliwa na watu
Mtu mwenye huzuni nyingi ajuaye sikitiko
Alikua mbele zake kama mche mwororo,
Na kama mzizi katika nchi kavu,
Hakuwa na umbo kuvutia wala uzuri
Hata tumwonapo tumtamani
Ni kama mtu ambaye watu humficha uso,
Wala hatukumhesabia kuwa kitu
Hakika amechukua masikitiko yetu,
Amejitwika huzuni zetu amejitwika.
Lakini na sisi tulidhani kuwa kapigwa,
Amepigwa na Mungu na kuteswa
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
Alichubuliwa kwa maovu yetu
Adhabu ya amani yetu ilikuwa kwake,
Na kwa kupigwa kwake yeye sisi tumepona
Sisi sote kama ko-ndoo tumepote
Kila mmoja njia yake yeye,
Bwana ameweka juu yake maovu yetu,
Alione-wa laikini alinyenyekea
Alionewa lakini hakufunua kinywa,
Kama mwanakondoo akipelekwa machinjio
Kwa kuonewa kuhukumiwa kaondolewa,
Ni nani atasimulia haya?
Ni nani aliyesadiki habari hii?
Na mkono wa Bwana amefunuiwa nani?