Verse 1
Aleluya tumwabudu Yesu Kristu
Yu hai mzima katika ekaristi
Aleluya aleluya aleluya
Verse 2
Sakramenti kuu hii ya mapendo,
Ulimojiweka kwa ajili ya watu,
Nasi twakupa yetu leo mapendo.
Verse 3
Ni sadaka ya msalaba twaijua,
Kafufuka kisha kapaa kwa Baba,
Yuko nasi katika hii Ekaristi.
Verse 4
Ni chakula chetu bora na kwa roho,
Ni Mwanakondoo yule wa pasaka,
Atulisha, atushibisha daima.
Verse 5
Njoni wote tumwabudu Yesu Kristu,
Nyoyo zetu, nyimbo zetu tumtolee,
Sifa zetu, shangwe zetu tumpatie.
Verse 6
Mwili wako uwe asili ya heri,
Utakase nyoyo zetu kwa damuyo,
Zifike mbinguni daima milele.n