Chorus
Aleluya tuimbe, Bwana amefufuka
Ametoka kaburini mzima, aleluya Bwana kafufuka
Kweli tuimbe aleluya *2
Verse 2
Kaburi liko tupu, Mwokozi ametoka
Ameshinda kifo na mauti, amefufuka aleluya
Verse 3
Mwokozi yu mzima kaburini hayumo
Ameshinda kifo na mauti, amefufuka aleluya
Verse 4
Tuimbe aleluya, tuimbe kwa furaha
Kwani Bwana ameshinda kifo, amefufuka aleluyan
Verse 5
Twendeni na mitume, twendeni Galilaya
Huko ndiko tutakapomwona, alivyosema aleluya