Ahadi

Ordinary TimeBible Procession
Verse 1

Niliyafumbua macho yangu na kutazama,

Ili nimuone ashukapo toka winguni,

Maana aliniahidi kuwa atarudi,

Kunichukua tukafurahi pamoja naye Mbinguni

Chorus

Ilikua hamu ya moyo wangu tazama

Na bado ninatamani kipi kitanizuia

Niuone uso wa Bwana na Mungu wangu

Nimuone akitimiza ahadi yake

Verse 3

Kaniahidi nikivumilia mpaka mwisho

Nitamuona katika kiti cha enzi

Akanionya nijitenge mbali na wazushi

Wasije wakaipotosha imani yangu, hakika

Verse 4

Nijapoanguka katika dhambi ya mauti

Ataiosha ikawa nyeupe kama suti

Na tena nikimlilia katika ukunga

Atanipa uzao kama nyota za mbinguni, ajabu

Verse 5

Kwa hiyo moyo wangu umetulia kabisa

Kwa kuwa nimejua kwamba ipo tumaini

Atukuzwe Baba Mwana na Roho Mtakatifu

Kama ilivyo mwanzo, sasa na mileleyote amina