Chorus
{Acheni mimi, nimuimbie muumba wangu,
Aliyeniumba, mimi kiumbe mwenye akili}*2
Aliyenipa uwezo wa kusimama hapa
Tangu tumboni mwa mama amenipa uhai
Juzi jana leo nimeamka kesho ajua yeye
Maisha yangu ayapa maziwa ni kama mtoton{Acheni mimi, nizitamke sifa za Mungu wangu
Na sitachoka, kumuimbia mimi ningali hai}*2
Verse 2
Nalala jioni na kuamka pia nazo nguvu,
Ninafanya kazi na kujipatia riziki zangu
Verse 3
Amenipatia akili yangu na wangu ubunifu,
Shuleni kazini ninayoyafanya hayana pungufu
Verse 4
Mara nyingi sana ninajiuliza nitampa nini,
Kwani Bwana amenitendea mengi bila ya kwa nini
Verse 5
Ninapokuwa nazo shida nyingi hunipa tulizo,
Kwake kila mara watu wote hupata burudiko.