SectionsBible ProcessionAcheni Kukata Tamaa

Acheni Kukata Tamaa

LentBible Procession
Chorus

{Mwenyezi ameniumba, akanileta kati yenu, Niwakumbushe watu wake thamani yenu duniani}*2n{Acheni acheni kufa moyo, Acheni acheni kukata tamaa, Yeye aliyewaumba anaijua kazi yake}*2

Verse 2

Aliijua siri yenu hata kabla hamjaumbwa,

Ramani ya maisha yenu, yote imo mikononi mwake

Magonjwa yanayowatesa na maumivu yasiyokoma,

Ni madogo kuliko yale aliyoyaponya kwa sekunde

Verse 3

Hali mbaya ya kiuchumi, mlo mmoja madeni mengi

Ni njia ya kunyenyekea na kumpa Mungu mkuu

Misiba inayowaliza mnapofiwa na ndugu zenu,

Ni njia ya wapendwa wenu kwenda mbinguni wakafurahi

Verse 4

Maumivu ya kuonewa kudhulumiwa kusingiziwa

Ni nafasi ya kusamehe na kujivika utakatifu

Matatizo ya ndoa zenu na migogoro ya familia,

Ni bahati mmejaliwa ya kujifunza uvumilivu

Verse 5

Bebeni misalaba yenu, nyamazeni msinung'unike

Huo ndio wokovu wenu shikilieni msiachie